Sura hiyo hapo juu ni ya mwanamke. Hebu itazame vizuri sana, kuanzia midomo, pua, macho na paji la uso. Hiyo ni sura ya mtu wa namna gani kitabia na je, umeshawahi kukutana na mwanamke mwenye sura kama hiyo? Kama umeshawahi kukutana naye, utajua kwamba, ninapozungumzia tabia na sura ninazungumzia jambo ninalolifahamu.
Wanawake wenye sura kama hiyo kwanza huwa wanaamini kwamba wana mikosi na kuamini kwao hivyo kunatokana na ukweli kwamba, mambo yao huwa hayaendi vizuri sana kwenye maisha. Kwa kifupi ni kwamba, wanawake wenye sura kama hiyo ni watu wa maumivu kimaisha.
Ni watu ambao kila wakati wamebeba lawama fulani na kila wakati wao ndiyo wenye kuonekana zaidi kwenye masuala ya uharibifu na ukosaji. Wanakuwa ni watu wakorofi kwa kiasi cha kutosha. Ni wapole au waongeaji sana, lakini ndani ya upole huo au uongeaji, wana visa vikubwa sana ambavyo hushangaza. Visa hivyo kwa sehemu kubwa ni ujeuri, utundu na ukorofi mwingine.
Mara nyingi, kwa nje wanaonekana kuwa dhaifu na hasa wale wenye maumbile marefu, lakini kwa kawaida wana nguvu sana. Kwa hiyo, kama ni kazi hufanya kazi kwa nguvu zao zote na kama ni kupigana hushinda sana kwa sababu wana nguvu. Mwanamke mwenye sura kama hiyo akiwa mrefu mwembamba, akiamua kutumia nguvu zake, siyo wanaume wengi watakaoweza kukabiliana naye, kwani ni wengi huchezea kichapo kama hawatajiandaa kikamilifu.
Wanawake wenye sura kama hiyo hawana ndoa imara kabisa na hata wanapokutana na wanaume ambao wanaweza kuwapenda, katika hatua za kujenga familia hujikuta wameharibu kila kitu. Hata hivyo, hata kukutana na hao wanaume wanaoweza kuwapenda siyo jambo rahisi.
Wanawake wenye sura kama hiyo hujichanganya sana linapokuja suala la shule. Badala ya shule, wengi hukimbilia mapenzi. Ukichunguza utakuta kwamba, wanawake wenye sura kama hiyo wengi wameanza uhusiano wa kimapenzi wakiwa wadogo bado. Kama wanatokea kuwa wazuri wa sura na umbo huandamwa sana kuliko wanawake wengine na hapo ndipo huzidiwa nguvu na kujikuta wakianza mapenzi katika umri mdogo. Ukiacha uzuri wa sura na umbo, wale ambao, hawajali kuhusu uzuri wao wakiamua kusoma, husoma hasa na kufika mbali na wanapojiajiri au kuajiriwa huwa ni wachapa kazi sana, ingawa huchukua muda kuona matunda ya kazi zao.
Kwa nje, ukiacha wale waongeaji, wale wapole ni wapole kweli, kwa sababu kuzungumza, ni suala gumu sana kwao. Huzungumza pale tu ambapo ni muhimu sana. Lakini haina maana kwamba wanawake wenye sura kama hiyo wote wana maumivu, hapana. Kuna wale ambao maisha yao ni ya amani, ingawa kwa bahati mbaya sana sijawahi kukutana nao.
Mdau - Mtambuzi
0 maoni:
Post a Comment