Tuesday 26 February 2013

TCRA yafunga Radio mbili na kuipiga faini CLOUDS

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka katika chanzo cha uhakika  ni kwamba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevifungia vituo viwili vya Radio ikiwemo Radio Iman ya mjini Morogoro na Radio kwa Neema ya Mwanza kwa muda usiopungua miezi sita huku Radio Clouds FM ya jijini Dar Es Salaam ikipewa onyo na kutakiwa kulipa faini katika kipindi cha mwezi mmoja. Chanzo chetu kimeendelea kutujuza kuwa Radio Kwa Neema FM Mwanza imefungiwa kwa Sababu ni kushabikia maswala ya uchinjaji Mwanza wakati Radio Iman FM ya Morogoro imefungwa kwa Kushabikia watu kutoshiriki Sensa 2012, Kwa upande wa Clouds FM wao wamepigwa faini kwa Kushabikia ushoga kwa kuendesha kipindi kisichofuata maadili cha Jicho la Ng'ombe.
Kwa hisani ya Chingaone blog

0 maoni: