Thursday 21 February 2013

Ogopa Dalali huyu ni TAPELI wa kutupwa


Jamani katika kutafuta nyumba za kupanga tuwe makini sana haza maeneo haya ya Sinza, Mwenge, Kijitonyama, Mbezi Beach, Mikocheni etc.



Binafsi na familia yangu tumetapeliwa 4 milioni mwezi huu wa kwanza. Kuna dadali mmoja ambaye ni maarufu kwa jina la DAUDI namba ya simu 0712-571827, huyu anaishi mjini kwa utapeli na ndiye aliyetutapeli sisi. Anatapeli kwa njia ya kukuonyesha nyumba nzuri sana ila cha ajabu anakutajia bei nafuu hadi utamshukuru Mungu kwa kukuwezesha kupata nyumba nzuri hivyo kwa bei nafuu namna hiyo, kwa kweli utasali na kusema hii ni bahati ya Mkenge. Sisi alituonyesha nyumba nyingi kuanzia mwezi wa 12 mwaka jana tulipoanza kutafuta nyumba,, tulimwambia atutafutie nyumba ya laki 4 - hadi 4 na nusu, aliweza kutupeleka nyumba kama 7 (nzuri za laki 3 - 4)bahati mbaya sisi hatukuzipenda hizo nyumba japo zilikuwa nzuri na kwa bei poa sana, hadi alipofanikiwa kutupeleka kwenye nyumba aliyotutapelia ambayo tuliona inatufaa.
Tulipoona nyumba inatufaa, tukamwambia atupeleke kwa mwenye nyumba, ambapo alitupeleka kwa mwenye nyumba FEKI, na tuliandikishana mkataba huu wa kikwetu wa shahidi wawili tukamalizana, ni kama wanakuwa na dawa maana siku zote sisi huwa tunalipa kodi wka cheki, ila this time hatujui nini kimetokea tukaamua kulipa CASH.

Anachofanya, yeye anajua nyumba inayopangishwa, anaenda pale anaongea na mlinz au aliyeachiwa funguo na kuwambia yeye ni dalali, ataleta mteja ila hata kama mteja akirudi baadae peke yake kuthibitisha bei asimtajie bei ya nyumba wala kutoa namba ya mwenye nyumba. Bahati mbaya zaidi tulipotapeliwa na kwenda kufungua kesi polisi, polisi walicheka na kusema huyu mwenye hii namba ni tabia yake, kwanza haitwi Daudi, tulipocheki namba yake kwa tigopesa, tulikuta amejisajili CECILIA MAKOYE. 

Ni mvumilivu kukufuatilia, hata ukisema hutaki hii nyumba wala hakulazimishi, na ukimwambia naomba namba ya mwenye nyumba uongee naye ili akupunguzie kodi, anakupa (ya matapeli wenzie) na kwa kuwa wewe huna jinsi ya kuthibitisha huyu ndo mwenye nyumba kweli, unakuwa huna jinsi zaidi ya kumuamini)



hapa tulipo hatuna pa kuanzia kumkamata na ndo tumeumia, 



Wanabodi, yaani sijui tunafanyeje ila tuwe makini kupita kiasi, maana huyu dalali mimi nilipewa na mtu ninayemheshimu sana hata nikashinda kumtilia shaka, ajabu hata aliyenipa anashagaa huyu dogo ni tapeli? polisi wanamjua na wanasema anakesi zaidi ya 10 za kutapeli watu hapo kituo cha kawe, ila ndo hivyo

Kama kuna yeyote anayemfahamu mwenye namba hii anisaidie, maana natamani sana nimpate ili niuone uso wake siku atakayoniona, japo najua hela haitorudi tena, ila lazima nimtie japo kilema.

Mdau  U Dar

0 maoni: