Tuesday 26 February 2013

Mtoko wa kwanza halafu hakupigii simu na anakata mawasiliano kabisa. Hizi zaweza kuwa sababu...!

Hizi zaweza kuwa sababu..........


1. Huenda kagundua kuwa una wivu kupita kiasi na unahisi kutokuwa salama kuwa naye
2. Au pengine ulikuwa na kisirani dhidi ya wahudumu wa mghahawa pasipo sababu
3. Uliuchapa mtindi kupita kiasi mpaka ukawa kero kwa kuongea sana bila mpangilio
4. Kwa muda mfupi kakugundua kwamba u-muongo, maelezo yako yanapishana sana
5. Umlalamishi, yaani kosa dogo tu lililofanywa na mhudumu wa mghahawa unalalamika muda wote mpaka inakuwa kero na kushindwa kujadili kilichowakutanisha…..

Hebu chunguza kama hizo sababu hazikuhusika…………..

Mdau Mtambuzi

0 maoni: