Thursday, 14 February 2013

Makongoro Nyerere kuunganishwa kwenye kesi ya Mauaji ya PAPA Musofe?

Mfanyabiashara, mkazi wa Dar es Salaam, Makongoro Joseph Nyerere, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shtaka la mauaji  ya mfanyabiashara mwenzake, Onesphory Kitoli.Aidha, Nyerere anatarajiwa kuunganishwa katika kesi hiyo na mtuhumiwa mwengine mfanyabiashara maarufu, Marijani Abubakari marufu kama Papaa Msofe (50), kwa mauaji hayo Februari 20, mwaka huu.
Jana saa 5:50, wakili wa serikali, Charles Anindo, alimsomea Nyerere shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi, Agnes Mchome. Alidai kuwa  Novemba 6, mwaka 2011 huko Magomeni Mapipa, Nyerere anadaiwa kumuua kwa makusudi Kitoli kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002. Anindo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na aliomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 20, mwaka huu, Nyerere atakapounganishwa na Papaa Msofe katika kesi hiyo.


Hata hivyo, Nyerere hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji hadi upelelezi utakapokamilika na itahamishiwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

Kwa hisani ya Chingaone blog

0 maoni: