Sunday 3 February 2013

Binti wa miaka 13afanyiwa Kitchen party

Baadhi ya watu waliokuwa kwenye sherehe hiyo

Hapa akiwa chini ya ulinzi akisindikizwa kwenye gari
Hapa akiingizwa kwenye gari kwa ajili ya kwenda kwenye kituo cha Polisi Stakishari
Hakuna lugha nyepesi unayoweza kuzungumza zaidi ya kusema haya ni maajabu ya mwaka 2013, kwani familia ya Masoud Kassim wa Karakata, Ukonga Dar imejikuta ikiingia kwenye mgogoro wa kisheria baada ya kuamua kumfanyia ‘kitchen party’  mtoto wao wa miaka 13 aitwaye Rafia Masoud, tayari kwa ndoa.

Tukio hilo la kusikitisha na kuhuzunisha limetokea Jumatano ya wiki iliyopita ambapo mtandao huu ulikuta Rafia akiwa katika sherehe hizo huku ndoa yake ikitarajiwa kufungwa jana  Februari 2.
 Kwa hisani ya GPL


0 maoni: