Tuesday 15 January 2013

Wahaya ni nomaaaaaaaaaaaa

Jamani tukubali au tukatake ila Wahaya kwa kujisifia ni nomaa, unaweza ukavunja mbavu kwa kucheka hasa pale unapofanya mazungumzo nao , yaani ni kosa kubwa kwao  kufanya mazungumzo na watu bila kujisifia, unaweza kushangaa hata issue ya msiba wao misifa full  hebu soma hapa .... Ni juzi tu nimesikia hii kwenye matangazo ya vifo.....!Ndugu Jestus Rweyemamu  wa Oysterbay  Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha  mtoto wake wa kiume Josephat  Jestus Rweyemamu  kilichotokea jana  huko Italia baada ya kupaliwa na Burger akiwa anaendesha gari yake mpya aina ya HAMMER  aliyonunua hivi karibuni, Msiba utafanyika kwa Shangazi yake huko Washingtown DC Marekani. Taarifa ziwafikie kaka yake mkubwa akiwa UK, dada yake mkubwa akiwa South Africa, ndugu yake wa mwisho akiwa Uswisi  bila kumsahau  pacha wake anayechukua Phd huko Austraria ............................. aaaaaaah jamani haya yote yanahusu? acheni hizo bwana....

0 maoni: