Sunday 30 December 2012

Salama Jabir, kwa hili jirekebishe!

Nafikiri wengi wenu mnaangalia kipindi cha  MKASI kinachorushwa na na kituo cha runinga cha East Africa TV (chanel5) kikiongozwa na mtangazaji wa kike nchini Salama Jabiri! kiukweli maudhui ya kipindi ni mazuri sana watu  kwani hupata fursa  ya kujua maisha ya watu mbalimbali maarufu hapa nchini hususan katika tasnia ya siasa,michezo,filamu,muziki nk....lakini tatizo lake kubwa ya kipindi hiki ni baadhi ya lugha  au matumizi yake  hasa ukizingatia kuna baadhi ya familia huangalia TV pamoja bila kujali umri , kiukweli inakera !!! mfano ni kipindi cha hivi karibuni Salama  wakati anafanya kipindi na Jackline Wollper wakati majadiliano ya kiendelea alisikika akimwambia John" umedinda" na hii ilitokea baada ya John kumtazama sana Wollper....  mwanzoni nilidhani  labda amepitiwa ila wakarudia tena safari hii ni Muba na John wakalitamka hilo neno! 
Angalizo
Jamani hata kama ni kwenda na wakati  inabidi pia tuangalie mila na desturi zetu  , cha ajabu na  kushangaza ni kwamba hizi vipindi vina wasimamizi hawalioni hilo? Ashakum si matusi kwa mtazamo wangu kuna baadhi ya neno hili si matusi lakini ifahamike kwamba kipindi hiki kinatazamwa na watu wa rika tofauti tofauti kuanzia wototo wadogo mpaka wazee! sasa jaribu kufikiri umekaa na mtoto na watoto wa siku hizi unawajua  unaangalia kipindi halafu akakuuliza hivi baba "kundinda"maana yake nini?  haya utamjibu nini?

0 maoni: