Friday 5 December 2014

Singasinga IPTL: Mimi ni mtanzania halisi, nimezaliwa Iringa


Mmiliki wa kampuni ya PAP inayodai kuinunua IPTL anayejulikana kwa umaarufu kama 'singasinga' kutokana na asili yake ya 'kihindi' amedai kuwa amezaliwa mkoani Iringa hivyo ni mtanzania halisi.

Singasinga huyo ambaye ni Harbinder Singh Sethi aliyasema hayo jana kwa vyombo vya habarii na amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya bunge kumtuhumu kuwa yeye ni mgeni aliyekuja kuihujumu Tanzania. Wapo baadhi ya wabunge ambao walinukuliwa wakisema kuwa wanampongeza mtanzania mwenzao yaani Rugemarila kwa kulipa kodi huku wakimponda vikali Sethi kwa kumtaja kama mgeni mwenye nia ya kulivurufa taifa.

0 maoni: