Thursday, 26 June 2014

Simulizi za Mapenzi : Safari yangu ya kuto kumwamini mwanamke katika mahusiano ilipoanzia.


Baada ya mahusiano ya miaka minne ya uaminifu na upendo kwa binti mmoja hivi jina kapuni, ndipo safari yangu ya kuto mwamini tena mwanamke katika mahusiano ilipoanzia kutokana na kile alichonifanyia.

Katika maisha yangu ya mahusino na huyo binti, nilikuwa mwaminifu sana pia nilimwamini kupita kiasi, siwezi sema labda sikuwa na uzoefu wa muda mrefu katika mapenzi laahasha, nilikuwa na uzoefu wa kutosha kuliko hata binti mwenyewe.


Kutokana na mazingira aliyokuwa ameyajenga kwangu ndio kilikuwa kichocheo kikubwa kilicho changia kumwamini kupita kiasi, Kwa uaminifu niliokuwa nao hata kama ungempiga picha akiwa nyumba ya kulala wageni(guest) ukaniletea ningekupinga kwa nguvu zote na kukuambia ni photo shop hiyo, unaweza kujiuliza labda alikuwa ananipa nini laahasha utajiumiza kichwa kwa kujiuliza maswali, maana kama ni mapenzi nilikuwa mkongwe kabla yake na nilikutana na wanaoyajua na kuyamudu hayo mambo ya kiutu uzima. Katika mapenzi binti alikuwa ni mgeni sana vitu vingi nilimpatia mafunzo kwa vitendo.

Kilicho kuja kubadilisha mtazamo wangu katika swala la uaminifu ilikuwa ni siku moja alipokuja kwangu, basi wakati nimekaa nae yapata mida ya saa nane mchana kuna mtu alikuwa anapiga simu yake, yule binti akawa hataki kupokea baada ya jamaa kukazana kupiga kama mara tatu nne hivi huku simu haipokelewi, ikanibidi nimuulize binti swali kwanini hapokei na ni nani ane mpigia, hapa nikapewa jibu jepesi, kwamba kuna jamaa anamtaka hivyo huwa anamsumbua kwa kumpigia simu, nikamuuliza swali la pili, je ulisha wahi kumwambia uko katika mahusiano, nikajibiwa ndiyo,haikupita muda akapiga tena nikapokea jamaa hakuongea baada ya kusikia sauti ya kiume, nikaamua kuishia hapo maswali yaliyo baki nikawa najiuliza mwenyewe na kujijibu.

Njia ya muongo ni fupi sana na siku zote ukiwa muongo usiwe msahaulifu, ilikuwa ya pata saa moja jioni kile kigiza cha usoni, nikaamua kwenda kuoga nikamuacha akiwa amejilaza kitandani, baada ya kufika bafuni nikagundua nimesahau sabuni chumbani, nilipofika mlangoni nikasikia kama binti anaongea na simu basi nikafungua mlango taratibu kwa kunyata kwa vile chumbani nilikuwa sijawasha taa kulikuwa na giza hivyo hakuweza kuniona.

Baada ya kuingia chumbani nikagundua alikuwa anaongea na yule jamaa aliekuwa akimpigia ile mida ya saa nane mchana, huku akimuuliza mbona ulikuwa haupokei simu na ninani aliepokea simu yako, binti alijitetea sana huku akimwambia ni binamu yangu, ulipopiga simu nilikuwa nae hivyo akasema ngoja leo akuzengue. Akamalizia na neno moja kwamba naomba uniamini.

Nilivuta pumzi nikapiga konde moyo nikingojea wamalize maongezi yao, baada tu ya kumaliza maongezi nikamuuliza binamu umemaliza kuongea, alishikuta sana alipogundua kwamba nilikuwa chumbani na nilisikia kila alichokiongea, alilia na kuniomba msahama, sikumsamehe kwa siku hiyo baada ya majuma mawili ya kujitafakari nikaamua kutoa msamaha, tukaendeleza safari yetu ya mahusiano iliyokatika behewa moja la uaminifu, likawa limesalia moja tu la upendo. UPENDO BILA UAMINIFU.

Basi hapo ndiyo mwanzo wangu ulipoanzia mpaka leo hii.

Uncle P wa JF

0 maoni: