Friday 30 May 2014

Fahamu utofauti wa maumivu ayapatao mwanaume na mwanamke pale wanapogundua kuwa wanasalitiwa

Wivu na maumivu anayoyasikia mwanamke pale anapohisi au kugundua kuwa mpenzi wake wa kiume anatembea nje ya mahusiano yao uko katika kiwango cha hisia “emotional level” wakati maumivu anayoyapata mwanaume kwa kusikia au kugundua kuwa mpenzi wake wa kike anamtu mwingine uko katika kiwango cha himaya “territorial level”. 

Wakati mwanamke anaumia kwa wivu akijiuliza kwanini mwanaume wangu achukuliwe na mwanamke mwingine, huku akiwa na kiu ya kumjua huyo mwanamke anafananaje? Ananini? Anauwezo gani kimvuto na kimuonekano? Maswali haya moyoni mwake huongeza maumivu katika hisia za mwanamke huyu, kwa upande wa pili mwanaume haumii kihisia lakini huumia na kupata machungu zaidi ya mwanamke huku moyoni mwake akihisi kushindwa kuimiliki himaya yake vema hadi mwanaume mwingine kuweza kuivamia, hujihisi kama askari aliye na silaha dhaifu au aliyeshindwa kutumia silaha zake vema hadi askari wa kambi nyingine akapata urahisi wa kumvamia tena kwenye kitovu cha kambi yake. 

Katika hali hizi, mwanamke humtazama mwanaume wake kama mpenzi wakati mwanaume akimtazama mwanamke wake kama himaya. Ni ngumu sana mwanaume kustahimili maumivu ya jinsi hii, na ndio maana kwa wanaume wengine huwa rahisi hata kuwaza kujitoa uhai au kuutoa uhai wa huyo mwanaume mwingine aliyetembea na mpenzi wake, wapo pia wanaume ambao huishiwa nguvu za kufanya tendo la ndoa kwa muda fulani “temporary impotency”mara tu wanapogundua kusalitiwa, na nimeshuhudia mwanaume aliyeamua kuzikata sehemu zake zote za siri kwasababu ya kuona hazina tena umuhimu, ingawa hakuweza kuishi tena baadae. 

Maumivu na matendo haya hayafanyiki sana kwa jinsia ya kike, wao huishia zaidi kulia, kupiga kelele sana, kutukana, na juhudi za kumsaka huyo mwanamke mwingine zikifanikiwa basi wanaweza kupigana kidogo na kuwekeana uadui wa kawaida, ambao sikumoja unaweza ukaisha 

Kwa hisani ya  Chris Mauki.

0 maoni: