Aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la Uganda UPDF, Generali David Sejusa(pichani) amezindua chama chake cha kisiasa nchini Uingereza na kumuonya Rais Yoweri Museveni kuwa utawala wake wa miaka 28 unaelekea ukingoni. Sejusa ambaye alikuwa jasusi wa zamani katika serikali ya Rais Museveni, amekiita chama chake "Freedom and Unity Front".
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda, serikali ya Uganda imepuuza uzinduzi wa chama cha Sejusa huku msemaji wa jeshi Paddy Ankunda akisema kuwa Sejusa anafamahu vyema kuwa amevunja sheria kwani bado hajasataafu kutoka jeshini.
Wakati sejusa alipohojiwa kuhusu uzinduzi wa chama chake, alisema kitaweza kuleta mageuzi. Alisema sio kwamba anataka kufanya hivyo lakini ikiwa Rais Museveni ataendelea kuwatesa watu, watafanya kila wawezalo kuweza kujilinda.
Mapema mwaka huu, generali huyo alitoroka Uganda kutafuta hifadhi Uingereza baada ya kuandika barua iliyokuwa na madai ya kutia wasiwasi mkubwa kuhusu serikali kupanga kuwaua wanajeshi wakuu wanaopinga mipango ya Rais Museveni kukabidhi mamlaka kwa mwanawe Brigedia Muhoozi Kainerugaba atakapoondoka mamlakani
Kwa hisani ya BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment