Friday 18 October 2013

Msaada ....Nimeambiwa na madaktari sina uwezo wa kuzaa (mbegu hazina nguvu)

Mimi ni kijana niliyeoa, niko kwenye ndoa sasa kwa miaka tisa (9) sijapata mtoto; vipimo vinaonyesha mke wangu hana tatizo lolote kwenye uzazi-ila tatizo ninalo mimi; nimeambiwa mbegu zinazozalishwa kwangu ni chache, pili hazina uteute utaozifanya ziteleze na kuweza kulifikia yai. Madaktari wanasema hakuna dawa ya kurekebisha hiyo kwani "production site ya viscosity is deady" Ila chakushangaza nina uwezo mkubwa wa kufanya tendo la ndoa hata mara tano kwa siku na zinatoka vizuri; na zilipimwa ni nzima kabisa tatizo ndio hilo "Uchache na no viscosity" Naombeni ushauri nifanyeje?

Uncle D

0 maoni: