Vijana wengi wa kiume hujikuta katika wakati mgumu kuchukua maamuzi ya kuishi na mwanamke japo yawezekana wakawa wanatamani kufanya hivyo kwa muda mrefu kutokana na vikinza vingi, vingine vikiwa ni vya kimaisha na vingine ni nadharia tu.Katika bandiko hili, nitagusia sababu kadhaa zinazochangia vijana wengi kujikuta wakisuasua au kuogopa kuingia kwenye ndoa.
1.Kupanda kwa gharama za maisha
2.Utitiri wa wanawake wanaopatikana kirahisi bila hata kuoa (Kwa kimombo hujiambia, “If I can get it for free, why buy it?”)
3.Maradhi hasa ugonjwa wa UKIMWI (Wengi hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa)
4.Kufurahia ‘uhuru’ [Hawa ni makapera wazoefu (wengine husema ‘bachela sugu’), hakuna mtu ambaye anaweza mshawishi akabadilisha maisha yake hayo ya kikapela (bachelor)]
5.Uhaba wa wanawake wanaofaa kuolewa
6.Kutopata ampendaye kwa dhati
7.Mahusiano mabovu ya awali
8.Kutoridhika na kipato chake (Hapa namaanisha pale ambapo mwanaume ana uwezo kabisa wa kuwa na mke na pia kuweza kukimu mahitaji yote pamoja na ya familia yake).
Malezi na Makuzi
1.Dhana mbovu juu ya ndoa (Kumekuwa na tabia ya watu kukatisha tamaa kwa kutoa vigezo, sababu, hadithi juu ya ndoa ambazo ni za kubomoa kuliko kujenga.)
2.Kuzaa ovyo/Kuzaa kabla ya ndoa (Kuna wanaume hadi anafikia umri wa miaka 30 tayari ana watoto wa wanawake tofauti hata watano na analea)
3.Kukua kwa idadi ya wanawake wanaotoka nje ya ndoa (Ni wanaume wachache wana kifua cha kuweza kuvumilia mkewe/mpenziwe kutoka nje na kuendelea kuwa naye)
Naomba tuungane katika mjadala, kupata mawazo zaidi, maoni, marekebisho na mengine mengi ambayo yanaweza kuwa msaada kwa mada hii.
Mdau - AshaDii.
0 maoni:
Post a Comment