Thursday, 26 September 2013

Ufuska wa kutisha

HAKIKA wazazi wanaosomesha mabinti lazima wataumia wakisoma kisa hiki kilichojaa ufuska wa kutisha, Amani linakupa kwa undani. Mwanafunzi wa kike aliyetajwa kwa jina moja la Agness, hivi karibuni alijifungia chumbani na njemba mmoja aitwaye Colvin na kufanya ngono zembe huku wakijirekodi na kujipiga picha za video wakidai ni kumbumbu yao.
Kisa hicho kinachoumiza kwa wazazi wanaolipa karo ili watoto wao wasome, kimetokea Kiwalani jijini Dar baada ya mwanafunzi huyo anayedaiwa kusoma chuo kimoja jijini humo kukacha masomo.

Inadaiwa kuwa binti huyo aliaga kwa wazazi wake kwamba anakwenda chuoni lakini hakufika na kukutana na mpenzi wake huyo na kujifungia chumbani.


Wakiwa chumbani kwa siku nzima wakifanya vitendo vingi vichafu ambavyo si rahisi kuviandika gazetini, hatimaye picha za video walizokuwa wakijirekodi zilivuja na kutua katika ofisi za gazeti hili.

Mwandishi wetu alianza kufanya utafiti na hatimaye kupata habari za Colvin ambaye inadaiwa kuwa ni mchezo wake kuwarekodi wanawake anaokuwa nao faragha. “Huyu jamaa amezidi, tumemuonya mara kadhaa lakini amekuwa mgumu, anawadhalilisha wanafunzi na wake za watu wakati mwingine bila ya wao kujua kama anawarekodi,” alisema mmoja wa watu wanaomfahamu kijana huyo.
Baada ya kupata habari hizo, paparazi wetu aliwatafuta wahusika wanaoonekana katika video hiyo ili kutaka kujua sababu ya kufanya hivyo.


“Ni kweli nilifanya hivyo, Agness ni mpenzi wangu, nimezaa naye, hivyo sioni ubaya kufanya mapenzi na mzazi mwenzangu huku tukijirekodi kama kumbukumbu yetu,” alisema Colvin na kukata simu huku akimtaka mwandishi wetu kutomfuatilia. 

Kwa upande wake, Agness awali alijaribu kutaka kumhonga mwandishi wetu fedha ili asichapishe picha hizo gazetini.
“Basi nikutumie hela usitoe hiyo habari na je, tukutane wapi ili nikupe hiyo hela…?” ilisomeka meseji ya Agness.
Msichana huyo alipoona kuna ugumu wa suala hilo kutimia akabadili maneno na kusema:
 “Kwani kuna ubaya gani kujirekodi tukifanya mapenzi na mwandani wangu? Kama amekuwa akifanya hivyo kwa wanawake wengine miye sijali,” alisema Agness.
Kama vile haitoshi, Agness akaanza kutukana matusi mazito kwa mwandishi wetu ambayo hayaandikiki gazetini. 


Kwa hisani GPL
Picha zaidi fungua hapa - Ufuksa wa Kutisha

Related Posts:

  • WEMA azua timbwili Wema Isaac Sepetu akiwa amefura kwa hasira. STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa vimbwanga, Wema Isaac Sepetu amezua bonge la timbwili kwa wafanyakazi wake wa ndani wa kiume na kike akiwemo mlinzi, Amani linakuletea kis… Read More
  • UDOM yaoza kwa tabia za kilaana - Wanafunzi wafumwa laivu wakisagana.... Hawa walifumwa laivu wakisagana nje ya hosteli yao............. Maadili yako wapi? Wizara husika inajua hili? … Read More
  • Full aibu PADRE afumwa laivu na mke wa mtu gesti KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu, Ijumaa Wikienda lina sakata zima.&… Read More
  • Mtawa Bandia atiwa mbaroni Iringa Taarifa za kipolisi, za kukamatwa kwa Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.  JESHI la polisi mkoa wa Iringa limemkamata mwanamke Phylis Wanjiru mwenye umri wa miaka 44 aliyevalia mavazi ya kitawa wa masister w… Read More
  • Shilole kaiba simu za Diamond? TAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.Msanii huyo alikumbwa na kas… Read More

0 maoni: