Thursday 12 September 2013

Mwenye nacho huongezewa ...... VODACOM yampa shavu Diamond


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom imeingia mkataba na msanii wa muziki wa Kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond’, kupitia wimbo wake mpya wa ‘My Number 1’. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa, alisema kuanzia sasa kampuni hiyo itahakikisha inashirikiana na msanii huyo katika kazi zake mbalimbali ambapo lengo kuu ni kutambua mchango wa wasanii nchini.

0 maoni: