Monday 9 September 2013

Mwili wa MWANAMKE aliyechinjwa kikatili na MUME wake waagwa

Picture
MAITI ya mwanamke aliyeripotiwa kuchinjwa kikatili na mwanaume aliyesadikika kuwa ni mume wake, Yusta Ernest (28), ameagwa kwa majonzi makubwa kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda mkoani kwa mazishi. Tukio hilo la kuagwa lilifanyika mapema leo hii katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar, na kuibua upya majonzi makubwa kwa ndugu na marafiki wa marehemu ambao wengi walionyesha wazi hisia zao kuwa wameumizwa na kifo cha kipenzi chao.

Akiongea kwa majonzi msemaji wa familia hiyo, Nelson Mgerwa alisema kuwa familia imeumizwa sana na kifo cha ndugu yao mpendwa ambaye ameondoka akiwa na umri mdogo. 
Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kuelekea Mpwapwa mkoani Dodoma, ambapo taratibu zote za mazishi zitafanyika katika kijiji cha Nzasa mkoani humo.

Angalia picha zaidi za tukio hapa chini

Mwili wa Marehemu Yusta Mkali ukiwa tayari kwa kuagwa Hospital ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam,na kuanza kwa safari ya mazishi yatakayofanyika kijiji cha Nzasa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Baadhi ya wafanyakazi aliokuwa akifanya nao kazi wakitoa heshima za mwisho


Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Yusta Mkali likifunikwa na kupandishwa kwenye gari tayari kwa kuanza safari ya kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi 


Mtuhumiwa Musa Senkando ambaye bado anatafutwa na Polisi 

Kwa hisani ya GPL / WAVUTI

0 maoni: