Wednesday 11 September 2013

Bibi harusi wa miaka 8 afariki baada ya kulala na mume wake wa miaka 40 usiku wa harusi yao....

Bibi harusi wa miaka nane huko yemen,amefariki dunia kutokana na michubuko ya ndani aliyoipata usiku wa harusi yake,alitoka damu mpaka kufa baada ya uke wake kutanuka kulikosababishwa na kufanya mapenzi na mume wake mwenye miaka 40. Mtoto aliyejulikana kwa jina la Rawan (pichani) ,alifariki huko Hajjah,Yemen kutokana na ripoti tulizonazo mtoto huyo alifariki jumapili,septemba 8.

Raia wema sehemu hiyo wanataka kukomesha suala hilo la kuoa wasichana wadogo na waliwaita polisi kuwakamata mume wa yule mtoto aliyefariki na familia yake. Lakini bado ndoa za wasichana wadogo za kulazimisha huko Yemen zinabaki kuwa utamaduni unaokubalika na jamii kwenye vijiji vingi.

Raia hao waliwaita polisi kuja kuwakamata huyo mume mkatili na familia ya mtoto na kuwapeleka kortini ambako haki itatendeka na kesi hiyo itawasaidia kukomesha uoaji wa wasichana wadogo kwenye nchi yao.

Mabloggers wa Kuwait wamemuombea 'bibiharusi' na kumlaani 'bwanaharusi' wakisema ni mnyama mkatili anayetakiwa kuadhibiwa vikali. Al Bawaba inaripoti kuwa zaidi ya robo ya wasichana wadogo huko Yemen wanaolewa kabla ya umri wa miaka 15. Inaongeza kuwa nchi hiyo ilipitisha sheria februari 2009 ambayo iliweka umri wa chini kabisa kuolewa ni 17 lakini hiyo ilikataliwa baada ya watengenezaji wa sheria kusema kuwa sio ya kiislamu.

Soma habari zaidi kwenye linki hizi hapa chini

0 maoni: