Wednesday, 26 June 2013

Baada ya Jeshi la Polisi kutoa kauli yake JOYCE KIRIA nae afunguka

Photo: MARAFIKI ZANGU NAOMBA NIWASHIRIKISHE PRESS YANGU NILIYOFANYA JANA.


                                                                                                                               24JUNE2013.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.                                    

YAH; KUOMBA MSAADA WANAWAKE WENZANGU NA WATANZANIA WOTE.

Jina langu ni Joyce Kiria, mke wa Henry Kilewo. Mimi ni mdau wa media, mdau wa Haki za Wanawake. Mume wangu ni mwanasiasa na ni mdau wa Haki za Binadam. Kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi tangu Ijumaa.

Mume wangu alipigiwa simu kutoka makao makuu ya jeshi la polisi wiki iliyopita. Yeye wakati huo alikuwa safarini kwa shughuli zake za kisiasa, akaniambia ameitwa na akawasiliana na mwanasheria wetu Peter Kibatala, mwanasheria nae alikuwa na shuguli nyingi wakakubaliana wakutane Dar ili waende kuitika wito huo. 21june2013 siku ya ijumaa mume wangu alikwenda makao makuu ya jeshi la polisi kuskiliza  wito huo. Mchana nikiwa naendelea na shughuli zangu za kikazi, nikapokea simu toka kwa wakili wetu Peter Kibatala akinijulisha ya kwamba wamemzuia mume wangu wakidai kwamba anahusika na kesi ya 2011 ya uchaguzi huko Igunga.

Baada ya kupokea hizo taarifa binafsi nikaanza kufatilia. Kwanza nikaanzia huko alikokuwa anashikiliwa (makao makuu ya jeshi la polisi) ambapo tulimkuta akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi chini ya askari SSP PASUA na wenzake. Nashukuru nilipata fursa ya kumuona na kumpa chakula ambapo mume wangu alikuwa hajala tangu asubuhi. Ilipofika saa moja jioni mume wangu Henry Kilewo alihamishwa kutoka makao makuu ya jeshi la polisi kwenda central polisi akalala pale.

Siku iliyofata nilidamka asubuhi nikampelekea chai. Chai ikapokelewa na askari akapelekewa akanywa. Baada ya muda mfupi akaingia SSP PASUA kutoka makao makuu ya jeshi la polisi, akazungumza na askari  wenzake ndipo niliporuhusiwa kumuona tena. Tukasalimiana kwa dakika mbili baada ya hapo akarudishwa lokap, basi na mimi nikaambiwa nimimi peke yangu naruhusiwa kupeleka chakula chake. Nikatoka kwenda kuandaa chakula cha mchana.

Ilipofika saa sita mchana nikawa nimefika central polisi kumpelekea mume wangu chakula.  Nilipata faraja sana baada ya kumkuta mwanasheria wetu Peter Kibatala akiongea na mteja wake ambae ni mume wangu Henry. Mwanasheria aliambiwa ampatie chakula lakini aonje kwanza. Baada ya kula na kuongea na wakili alinisalimia kwa mbali akarudi zake lokap. Wakati naondoka central nikaambiwa na askari wa zamu kwamba chakula cha jioni ni saa kumi na moja kamili mwisho kumi na mbili kamili. Ilipofika muda huo nikawa central cha chakula changu.

Wakati napanda ngazi kuelekea mapokezi ya central polisi, askari mmoja akaanza kusema ya kwamba huyo mnaempelekea chakula kashachukuliwa. Mi nikasogea mpaka mapokezi, nilipofika mapokezi nikamkuta askari ambae alikuwepo tangu asubuhi, nilimueleza ya kwamba nimemletea mume wangu chakula cha jioni. Askari akanijibu ya kwamba ‘’MTU WENU KASHACHUKULIWA’’ nikauliza wamemchukua wamempeleka wapi? Akanijibu ‘’HATA MIMI SIJUI’’ 

Baada ya kupata hayo majibu toka kwa askari wa zamu, nilimpigia wakili wetu Peter Kibatala kujua mume wangu amepelekwa wapi. Cha ajabu wakili nae alipata mshituko na akaniambia kwamba na yeye hana taarifa zozote na anashangaa kwa nini wamemtoa bila kumpa taarifa yeye kama wakili wake. Ndipo hapo nilipopata maswali mengi ambayo sipati majibu mpaka sasa.

Ndo sababu hasa ya kuita vyombo vya habari mnisaidie, na watanzania pia mnisaie, wanawake wa nchi hii mnisaidie zaidi ya hao Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mh IGP Mwema mnisaidie. 

1. kwanza kumuombea mume wangu huko aliko aweze kuwa salama. 

2. Ni kweli sijui sheria, lakini  inawezekana vipi mtuhumiwa ambae yuko chini ya ulinzi wa jeshi la polisi  atoke bila askari wa zamu kujua?

3. Mimi sina tatizo na mume wangu kutuhumiwa, lakini kinachoniuma zaidi ni kwanini inakuwa siri?

4. Mimi ninataka kujua mume wangu yuko wapi? Najua anashikiliwa na jeshi la polisi, nachotaka kujua yuko wapi? Au sina Haki ya kujua?

5. Wanawake wa nchi hii nisaidieni, tunateseka na watoto wangu tukitafuta kujua mume wangu baba yao yuko wapi? Ndugu zake wananiuliza, mama yake, baba yake, marafiki wananiuliza Henry yuko wapi? Kwa nini wananificha mimi mke wake?

6. kuna Agenda gani ya siri, Wanawake wenzangu, yanapotokea matatizo sisi ndiyo wahanga pamoja na watoto wetu, mfano halisi ndo huu kama mnavyoniona na watoto wangu. Kitendo cha kufanya jambo hili siri nimeishiwa maziwa ya kumnyonyesha mwanangu mchanga Linston.

Naomba muungane na mimi katika kipindi hiki kumuombea mume wangu Hanry Kilewo avuke kizingiti hiki kinachomkabili.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA


JOYCE KIRIA
WANAWAKELIVE
Baada ya Jeshi la polisi kupitia msemaji wake kutoa kauli yao baada ya Joyce Kiria kuita waandishi wa habari na kuongea nao kuhusu sakata la kutojua mumewe alipo   Joyce Kiria aamua kuweka bayana yaliyo moyoni kupitia ukurasa wake wa Facebook ....... Nanukuu

Binafsi kama JOYCE KIRIA nachukua nafasi hii tena kumuomba msemaji wa jeshi la polisi anisamehe kama nilikosea kudai haki yangu na watoto wangu ya kujua baba yao/ mume wangu yuko wapi! taarifa nilizokuwa nazo hazikuwa na uhakika kwani kuna waliosema kapelekwa Igunga na wengine wakasema kapelekwa Tabora. kwanini niishi kwa mashaka na taarifa zisizo rasmi toka kwa watu baki wakati waliomsafirisha Jeshi la polisi walikuwa na uwezo wa kuitaarifu familia au wakili wake?

Narudia tena kama ni makosa NAOMBENI MSAMAHA KWA MH RAIS, IGP MWEMA, WANAWAKE WA NCHI HII NA WATANZANIA WOTE.


Soma habari zinayofanana na hii hapa chini


0 maoni: