People's Magazine

The place where you can find everything...

Wednesday, 15 May 2013

Namfuata MWISHO Namibia


LICHA ya Mwisho Mwampamba kuwa mume wa ndoa wa Meryl Shikwambane, msanii wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha amesema anajiandaa kwenda nchini Namibia wanapoishi wanandoa hao kwa lengo la kujumuika na Mwisho na kula bata.


Akizungumza na Risasi Mchanganyiko jijini Dar es Salaam, Baby alisema bado ana uhusiano wa kimapenzi na Mwisho na kwamba yeye ndiye alimwalika aende Namibia wakafurahie penzi lao.
“Nakwenda Namibia kwa Mwisho wangu. Simwogopi huyo Meryl, kwanza yeye ndiye aliyeingilia penzi langu. Mimi ndiye wa kwanza kuwa na Mwisho, hivyo ni halali yangu.

“Mwisho mwenyewe ndiye aliyeniambia niende na amesema nitafikia hotelini, nitafurahi naye kwa muda wote nitakaokuwa huko, mambo mengine mwenyewe ameshayapanga na atajua cha kufanya.”


Kwa hisani ya GLP

Unknown kwa 12:04
Share

No comments:

Post a Comment

Toa ushauri wako au andika chochote hapa ... Leave your comment here

‹
›
Home
View web version
Powered by Blogger.