Monday 1 April 2013

Simba yatenga million 25 kwa ajili ya KASEJA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, wametenga kitita cha dola 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 25) ili kipa wao, Juma Kaseja aongeze mkataba.  

Awali kulikuwa na taarifa kuwa kipa huyo atatemwa Msimbazi baada ya kuwasili kwa Abel Dhaira ambaye ni kipa namba moja wa timu ya taifa ya Uganda. 

Simba imegundua umuhimu wa Kaseja na imetangaza kumsainisha mkataba mpya kwa kitita hicho, ikiwa ni siku chache baada ya kipa huyo kutangaza kuwa yupo tayari kufanya mazungumzo na klabu yoyote.
Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya kamati ya usajili ya timu hiyo, kimelithibitishia Championi Jumatatu kuwa kiasi hicho kimetengwa kwa ajili ya kuhakikisha Kaseja anabaki Simba.
Chanzo hicho kilisema wanaheshimu uwezo wa kipa huyo, hivyo wameona ni vyema abaki kikosini ili asaidiane na Dhaira.
“Katika kuhakikisha tunambakiza kipa wetu Kaseja, tayari tumemuandalia dola 20,000 ili aendelee kubaki kuichezea Simba msimu ujao.
“Tumeridhishwa na kiwango chake ndani ya uwanja, tunaamini ni kipa bora mwenye uwezo mkubwa golini, hivyo atabaki asaidiane na Dhaira,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa ofisa habari wa timu hiyo kuhusiana na taarifa hizo, alisema: “Muda wa usajili bado, ni vyema tukasubiri kwanza, kila kitu tutakiweka wazi usajili ukifunguliwa.”

Kwa hisani ya GLP

0 maoni: