Saturday 6 April 2013

Mzee Mangula kufunga ndoa na mwalimu leo...

Mwanasiasa mkongwe, mwadilifu, asiyependa makuu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Phillip Mangula anatarajia kufunga ndoa leo tarehe 6/4/2013 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini, mjini Njombe.Mzee Mangula anafunga ndoa na Yolanda Kaberege Mkuu wa Sekondari ya Philip Mangula, iliyopo wilayani Wanging’ombe, mkoani Njombe. 

Hatua hiyo ya Mzee Mangula kuoa inakuja baada ya aliyekuwa mke wake kufariki dunia mwaka 2004, kutokana na ugonjwa wa saratani.

Msemaji wa familia ya Mzee Mangula ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) tawi la Njombe, Dk Lechion Kilimike alilieleza Mwananchi kuwa ndoa hiyo itaongozwa na Askofu Mstaafu wa Kanisa hilo, Solomon Swalo.

Dk Kilimike alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ,Waziri Mkuu Pinda anatarajiwa kufuatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali walioalikwa kwenye sherehe hiyo.

0 maoni: