Wednesday, 24 April 2013

Ndoa yangu haivunjiki leo wala kesho..... Aunt EZEKIEL

MWANADADA anayetamba katika filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa ndoa yake haiwezi kuvunjika leo wala kesho kwani amejipanga kikamilifu. Aunt aliyasema hayo kwa madai kuwa watu wengi wamekuwa wakitaka kushuhudia ndoa yake na mumewe, Sunday Demonte ikivunjika lakini yeye ana uhakika kuwa haitavunjika milele kwani maisha anayoishi sasa siyo sawa na yale ya zamani. “Naweza kusema kuwa ndoa yangu itadumu milele na haivunjiki leo wala kesho kama wengi wanavyosema, ninajua ni kitu gani  ninachokifanya, nimebadili mwenendo wa maisha yangu, pia ninajiheshimu kama mke wa mtu,” alisema Aunt.

Kwa hisani ya - GLP

0 maoni: