Tuesday 30 April 2013

Msigwa chaliii...

Msigwa alipiga mikwara kuwa hotuba yake itakuwa babkubwa, itatetemesha, itakuwa kombora. Hali hiyo ni tofauti na hotuba yenyewe ambayo ililazimika kubadilishwa baada ya kuvuja na kusambaa kwenye mitandao. Hotuba hiyo imekuwa TUPU. Haina chochote cha kusisimua. Kombora moja tu la Dr.Nchimbi limeisambaratisha hotuba nzima na Msigwa ameonekana akiwa na sura ya kuona aibu.

Jitihada za tundu Lissu kutaka kumuokoa Msigwa hazikuzaa matunda.

Kiujumla Msigwa leo ametia aibu kubwa.

Kwa kuelewa zaidi utupu wa hotuba ya Msigwa angalia hii checklist:

1. Je, umeona taarifa yoyote mpya kwenye hotuba ya Msigwa?

2. Je, umeona utatuzi wowote wa changamoto za kitaifa kwenye hotuba hiyo?

3. Je, kusomwa kwa hotuba kama hii kunaweza kubadilisha nini nchini?

4. Je, hotuba hii isingesomwa kuna jambo lolote lingeharibika?

5. Je, hotuba hiyo imemuwezesha mwananchi kujua kama kiwango cha fedha zilizotengwa kwenye wizara husika kinatosha?

6. Je, hotuba hiyo imekuwezesha kujua meneo gani yanatakiwa kupewa vipaumbele na wizara hiyo katika mwaka huu wa fedha?


Picha kwa hisani ya - mbungeiringamjini blog

0 maoni: