Monday, 1 April 2013

Jinsi ya kuondoa madoa yaliyosababishwa na CHUNUSI

How to Get Rid of Pimple Scars Naturally
Asilimia kubwa ya watu wamekuwa na tatizo la kuwa na makovu yanayosababishwa na chunusi kwa kipindi kirefu bila kupata ufumbuzi,  na hii husababishwa  sana na mabadiliko ya miili kipindi cha ujana , au kwa watu wenye nyuso zenye mafuta na baadhi ya watu wamepata matatizo haya  baada ya kutumia baadhi ya vipodozi visivyoendana na ngozi zao. Tatizo hili limekuwa kubwa kwa baadhi ya watu na kuna wakati mtu ana kosa hata raha na kuwa huru  kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na mtu kwa kuogopa muonekano wa madoadoa ya ngozi ya uso wake. Leo  tutaenda kuangalia  moja ya tiba ya kuondoa madoa madoa ya chunusi inayoweza kutengenezwa na mtu yoyote nyumbani bila kutumia gharama kubwa.

Mahitaji
Unga wa Riwa
Maji ya Rose (Rose water)
Maji safi ya kawaida
Limao
Mafuta ya Olive (Olive oil)

Hatua ya Kwanza
Chukua unga wa Riwa na Maji Rose uyachanganye  pamoja na ukoroge hadi mchanganyiko wako uwe mzito.

Hatua ya Pili
Upake mchanganyiko wako katika sehemu yenye makovu na uache hadi ukauke. Unaweza kukaa na huu mchanganyiko huu kwa muda mrefu  ila inategemea na nafasi yako pia, mchanganyiko huu unasaidia kunyonya mafuta na kuacha ngozi kavu.

Hatua ya Tatu    
Nawa  vizuri na maji ya uvuguvugu.

Hatua ya Nne
Paka Juice ya Limao kwenye sehemu yenye makovu.  Juisi ya limao inatumika kama brichi ya asili ambayo husaidia kufifisha madoadoa  na kuondoa makovu kwenye ngozi .

Hatua ya Tano
Paka mafuta ya Olive  kwenye makovu, hii husaidia kulainisha ngozi na kufanya makovu yasionekane kirahisi.

Mambo ya kuzingatia
Wakati unaanza kufanya tiba hii jaribu kuacha kutumia aina ya vipodozi vya kemikali ulivyokuwa unatumia na utumiea hii tiba ya asili isiyo na madhara. Jaribu kufanya zoezi hili walau mara mbili kwa wiki  ndani ya mwezi mmoja utaona matunda yake.

0 maoni: