Saturday 27 April 2013

Dr. CHENI apata BINTI

STAA wa filamu za Kibongo nchini, Mahsein Awadh ‘Dokta Cheni’ amejawa na furaha baada ya mkewe, Sabra kujifungua mtoto wa kike juzi kwenye hospitali ya TMS iliyopo Mbezi Tankibovu jijini Dar. Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Dokta Cheni alisema kuwa amefurahi kuongeza mtoto wa pili kwani amekuja wakati muafaka kama alivyokuwa amepanga.


“Nilimuomba Mungu iwapo mwanangu wa kwanza Abdulmalick atafikisha umri wa miaka mitano, basi nipate mwingine na ikiwezekana awe wa kike, kweli Mungu amesikia maombi yangu na kunijalia leo hii, namshukuru sana,” alisema Dokta Cheni.


Cheni aliweka wazi furaha yake hiyo kwa kusema kwamba mtoto huyo amekuja kama ‘suprize’ kwani alitarajia angezaliwa Mei mwaka huu kama mkewe alivyopangiwa na daktari.

Aidha, alisema kuwa ujio wa mtoto huyo umekuwa wa ghafla kwa sababu mkewe alikwenda hospitali kwa ajili ya kutibiwa vidonda vya tumbo lakini alipofika akafanikiwa kupata mtoto.

“Mimi na mke wangu hatukutarajia kupata mtoto leo lakini tulipofika hospitali daktari alisema mke wangu yupo tayari kwa ajili ya kujifungua na kweli baada ya muda mfupi akajifungua kwa njia ya kawaida,” alisema kwa furaha.

Cheni alimalizia mazungumzo na safu hii huku akikimbia kwenda kumfanyia ‘shopping’ mtoto wake huyo.


Picha zaidi bonyeza hapa - Dr. CHENI

0 maoni: