Monday 11 March 2013

Wanawake wenye sura hii, kwa kuibua wanaume ‘mabomu’ ndio wenyewe…!

Hiyo sura unayoiona hapo juu ni ya mwanamke, ambaye amejiremba na kupendeza. Lakini kujiremba kwake hakujabadilisha sura yake halisi, kwani hata bila kujiremba angeweza kuonekana kama anavyoonekana hapo. Kwenye sura hiyo, naomba uzingatie sana midomo, mashavu na macho. Kwa ujumla kwa mujibu wa mazoea yetu kuhusu uzuri wa mwanamke, tunaweza kusema, sura hiyo ni nzuri.
Wanawake wenye sura kama hiyo, hushikwa haraka na mashaka na kubabaika kwenye maisha. Ni wanawake wanaopenda kujilinganisha na kujiwekea thamani kwa kadiri ya jinsi wanavyohisi wakijilinganisha na wengine. Katika hali hiyo, ni wanawake ambao mara nyingi wako kwenye kusongeka.


Ni wanawake ambao ndoa zao huwa na mashaka makubwa, kwani katika kutojiamini kwao na kuingia mara kwa mara kwenye kusongeka huwafanya waume zao kuhisi kero na usumbufu wa mara kwa mara. Naweza kusema, huwa wanazivuruga wenyewe ndoa zao.

Lakini ni wanawake wapole wasiopenda sana kusema. Kwa bahati mbaya, wanapochokozwa, huwa wakali sana na wanaojua ‘kukandia’ hasa. Wana kawaida ya kupuuzia kwa wazi, yaani kumdharau mpenzi huku akijua kwamba anadharauliwa.

Wanawake wenye sura hii mara nyingi ni watu ambao wanayatazama maisha kupitia tundu jembamba sana. Wanayaona maisha kama kitu fulani kimoja tu ambacho kikiharibika au kisipoenda sawa, basi. Wanaweza kuwa wanayaona maisha kama kazi yao, maisha kama watoto, maisha kama ndoa, maisha kama biashara zao na vingine kama hivyo.

Kwa sababu hiyo huwa wanajali sana kitu au vitu fulani tu kwenye maisha, kuliko vingine. Jambo hili huwafanya kuwa wanawake wanaomudu sana kwenye eneo moja na kushindwa kabisa kwenye maeneo mengine. Kwa mfano, unaweza kukuta anashirikiana vizuri sana na wafanya bishara wenzake wakati haelewani na jirani au mume au ndugu.

Ni wanawake wenye huruma, hasa kwa wenzao ambao hawawazidi. Wanapenda sana kujitolea katika shida kama misiba na kusaidia sana pale ambapo kumetokea tatizo la kijamii. Wanaweza sana kujishusha ikiwa ni njia yao ya kutaka wasiingizwe kwenye mashindano kwa sababu ingawa wanaishi kwa kushindana, bado wanaogopa kushindana kwa wazi.

Ni wanawake wenye ufahamu ambao pia wanapofanya jambo hufanikiwa, kwani ni wapaniaji ambao hufanya mambo yao polepole lakini kwa uhakika. Kama wamefanikiwa na kumudu kuishi bila kujilinganisha (siyo mara nyingi), huwa ni wanawake ambao kila mmoja anaweza kupenda kuishi au kufanya nao kazi.

Kwenye masuala ya uhusiano, wana dharau na kujiona kuwa bora sana. Ni katika mkabala huo ambapo hunasa kwenye tundu bovu. Hebu jaribu kumkumbuka mwanamke unayemjua mwenye sura kama hiyo, halafu umkague mpenzi wake. Kwa kawaida wanakuwa na wapenzi ‘mabomu.’ 

Kwa ujumla kama wamefundishwa kujiamini huwa ni wanawake wazuri na wenye kumudu kujenga familia bora sana.

Kwa hisani ya Mrembo by Nature .......

0 maoni: