Saturday, 5 January 2013

WOLPER ageuka gumzo kwenye msiba wa SAJUKI

JACQULIENE Wolper amekuwa gumzo katika msiba wa staa mwenzake wa filamu za Kibongo, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ baada ya kutinga msibani kama vile anakwenda harusini. Wolper alitinga msibani juzi pande za Tabata Bima jijini Dar saa tisa alasiri akiwa amevaa nguo ndefu  bila ya kutupia mtandio wala khanga kichwani kwake.

Baadhi ya waombolezaji, walimshangaa staa huyo kwa kushindwa hata kujitanda mtandio kama walivyofanya wasanii wengine.

 “Hivi Wolper hajui kama msibani watu wanatakiwa kufunika kichwa kwa khanga au kwa mtandio? Mbona amekuja kama mtalii? Huu uzungu sasa umezidi, halafu si alibadilisha dini huyu?” alisikika muombolezaji mmoja.
Akiwa katika hali hiyo, Wolper aliyeongozana na Irene Paul alienda kuwapa pole wafiwa kwa kuanza na mama mzazi wa Sajuki, mke wa marehemu, Wastara na  kuangusha vilio Wastara akimshukuru kwa kumpa moyo wakati wa kumuuguza mumewe.

Kwa hisani ya http://www.globalpublishers.info


0 maoni: