Tuesday, 8 January 2013

POLISI agombea Mwanamke auawa...............



ASKARI wa jeshi la polisi aliyetokea mkoani Dodoma alikokuwa anafanyia kazi kuja kwenye mapumziko ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya  mkoani Iringa mwenye namba G. 3679 PC Manase Samwe (23), amefariki baada ya kupigwa na marungu hadi kufa na walinzi wa misitu ya Sao Hill, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema askari huyo aliuawa kwa kipigo na mgambo kutokana na kugombea mwanamke aliyekuwa akimnywesha pombe za kienyeji.

Chanzo cha askari huyo kupata kipigo kutoka kwa mgambo hao ambao ni walinzi wa misitu ya Sao Hill, imedaiwa kuwa ni mwanamke ambaye askari huyo awali alikubaliana naye kwenda kufanya naye mapenzi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi, suala ambalo lilipingwa na dada wa polisi huyo.

Chanzo cha habari kinasema dada wa Samwe hakutaka kaka yake aondoke na mwanamke huyo kutokana na tabia yake ambayo aliiona siyo nzuri lakini polisi huyo hakusikia akawa anamng’ang’ania.

Akizungumzia tukio hilo wiki iliyopita ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda (pichani juu)  alisema kuwa tukio hilo la kupigwa hadi kufa kwa askari huyo lilitokea kwenye kilabu cha pombe za kienyeji cha Lusasi kilichopo eneo la Sao Hill, Tarafa ya Ifwagi wilayani Mufindi baada ya kutokea mvutano kati ya askari na mwanamke huyo
 “Baada ya dada wa askari huyo kuona kuna mvutano mkubwa kati yao, aliwaita mgambo wa Kijiji cha Mapogolo na walipofika hawakuuliza chanzo ni nini, walianza kumpiga askari huyo kwa marungu na baada ya kuzidiwa alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mufindi ambako muda mfupi baadaye alifariki dunia,” alisema Kamanda Kamuhanda.

 Aliwataja waliokamatwa kutokana na mauaji hayo kuwa ni Leonard Samwel (52), Isaack Sagala (36),  Eleuteri Sengala (41), Wilbert Ngailo (31), Greyson Sagala (27) na Dickson Makombe (30), wote ni walinzi wa misitu ya Sao Hill na mwanamke aliyekuwa pamoja na askari huyo.


Kwa hisani na http://www.globalpublishers.info

0 maoni: