Maafisa wa Fifa akiwemo Rais wa chama hicho,Sepp Blatter(kushoto) na Michel Platini(Kulia) wamehojiwa kuhusu uhalali wa mkataba wa kuandaa michuano ya Kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 kwa Urusi na Qatar. Rais wa Fifa, Blatter na Platini wa shirikisho la soka barani ulaya Uefa, walishiriki katika mchakato huo mwezi Desemba mwaka 2010.Mkuu wa kitengo cha upelelezi ndani ya Fifa anafanya uchunguzi namna ambavyo mchakato huo ulifanyika.
umla ya Wajumbe 13 kati ya 24 waliokuwa kwenye kamati wamekuwa wakihojiwa kuhusu sakata hilo.
Baadhi ya walioshiriki kupiga kura wamestaafu huku wengine wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa halikadhalika kushinikizwa kuacha kazi baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja sheria ya Fifa.
Hatua hii haina uhusiano na uchunguzi uliofanywa na gazeti la Daily Telegraph kuhusu maafisa wa zamani wa Fifa, Mohamed Bin Hammam na Jack Warner wanaohusishwa na utoaji wa mkataba wa kuhodhi mashindano ya Kombe la dunia kwa Urusi mwaka 2018 na Qatar mwaka 2022.
Juma hili, gazeti hilo limeeleza kuwa shirika la upelelezi FBI linachunguza malipo yanayodaiwa kutolewa na Kampuni ya Bin Hammam kwa Warner na Watoto wake muda mfupi baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika.
Kwa hisani ya BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment