Sunday 2 February 2014

HAYO NI MAMBO 10 YA KUMTAMBUA YULE MPENZI WAKO KABLA HAMJAFUNGA PINGU ZA MAISHA NAYE

Habarini marafiki zangu


Marafiki zangu nimeona nishare nanyi hii kitu kwani nimeisoma mahali nikaona nanyi itawafaa pia kuisoma na ndipo nimedadavua huko na kuileta hapa jamvini nanyi mpate kitu toka hapa Zifahamu tabia za mpenzi wako mapema na kugundua  ukorofi wake mapema kabla hamjafunga NDOA
Dalili:

1. Mpenzi wako anakuwa na wivu sana kwa ule muda unaotumia kuwa na wafanyakazi  wenzako, marafiki na hata ndugu zako, ingawa sio kwamba anataka muda huo awe na wewe.

2. Anakuwa na tabia za kukuudhi na kukutawala, ataangalia sana kutoka na kuingia kwako,  nyendo zako na hata matumizi yako ya fedha, na kama ukimuuliza kwanini anafanya hivyo 
atajiteteta kuwa anakusaidia kufanya maamuzi sahihi.

3. Taratibu anakutenga na wote waliokaribu na wewe, pia anajaribu kukutenga na wale  wanaoonekana kuwa msaada kwako kama vile wale unaowasiliana nao kwa simu, wafanyakazi wenzako na hata ndugu zako wa karibu.

4. Huwa na tabia ya kuwalaumu sana wengine kwa matatizo anayoyapata yeye.  Mfano anapokosa kazi, anaposhindwa shuleni, anapokosa pesa nk. Kila kitu ni kosa la  mtumwingine na sio yeye.

5. Hukasirishwa na kuudhiwa na vitu vidogo vidogo na vya kawaida katika maisha ya kila siku, 
mfano akiambiwa afanye kazi zaidi ya muda wa ofisi, akiombwa amwangalie mtoto, anapopingwa katika kitu kidogo nk.

6. Anakuwa na tabia za kikatili kwa wanyama wafugwao “pets” na hata kwa watoto.  Haumizwi pale anapoona maumivu au kuteseka kwa kiumbe kingine. Anaweza kujiona  anacheza au anatania bila kujua anamuumiza mtoto au mnyama.

7. Ni wenyetabia ya mabavu hususani katika tendo la ndoa, hawatojali hisia zako, umelala usingizini au unaumwa, bali hujali zaidi kuzitimiza haja zao.

8. Ni wenye maneno makali yakuumiza na ya kushusha hadhi, huweza kukuamsha usingizini ili akutukane au kukugombeza. Akianza malumbano hakupi upenyo wa kwenda kulala,  anaweza kulalama usiku mzima.

9. Sio watu wakutabirika, ni watu wenye hisia za kubadilika badilika, mara muda huu  anafuraha na kuonyesha mapenzi, mara ghafla kakasirika na kutaka kuadhibu mtu. 

10. Anaweza akawa na historia ya tabia za kikorofi na kigomvi, labda amewahi kuwa na  matukio ya kuwapiga marafiki zake, akijitetea kuwa alipitiwa tu na hasira

0 maoni: