Rais Goodluck Jonathan ameidhinisha sheria inayotoa adhabu kali kwa wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja
Maafisa wakuu Kaskazini mwa Nigeria, wanasema kuwa wamewafikisha katika mahakama ya kiisilamu wanaume 11 wanaoshukiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Kamishna mkuu wa sheria za kiisilamu katika jimbo la Bauchi, alisema kuwa wanaume hao walizuiliwa mwezi jana na ikiwa watapatikana na hatia huenda wakahukumiwa kifo kwa kupigwa mawe.
Walisema kuwa mmoja wa washukiwa ambaye ni mkristo, atashitakiwa katika mahakama nyingine ya kiserikali.
Aidha kamishna amekanusha madai kuwa wanaume hao waliteswa wakiwa wanazuiliwa.
Mapema mwezi huu Rais Goodluck Jonathan alitia saini sheria inayotoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Afisaa mkuu wa haki za binadamu katika umoja wa mataifa, Navi Pillay aliikosoa sheria hiyo kwa kusema imehatarisha zaidi maisha ya wapenzi ya jinsia moja nchini Nigeria.
Kwa hisani ya BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment