Wednesday, 18 December 2013

Majambazi yawabaka mama, wanawe watatu

Watu  wanaokadiriwa kufikia saba wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na mapanga na marungu, wamevamia nyumbani kwa mkazi wa kijiji cha Kaduda kata ya Katoro wilayani Geita na kuwabaka kwa zamu mama na wanawe watatu kwa zaidi ya saa mbili. Hali kadhalika, watu hao walimjeruhi mmoja wa watoto wake wa kiume aliyekuwa akishuhudia unyama huo ukifanyika.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 15, mwaka huu baada ya kuvamia na kuvunja mlango wa nyumba walimokuwa wamelala wakati baba mwenye mji huo akiwa safarini.

Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Jumanne Faida, alisema baada ya kutekeleza ukatili huo, mama na watoto hao walipiga yowe kuomba msaada.

Faida alisema kuwa watu hao walikuwa wakimbaka mama huyo na wanawe hao wenye umri wa kati ya miaka 14, 10 na 17 kwa kupokezana mbele ya mtoto  wa kiume ambaye walimjeruhi kwenye paji la uso kumcharanga kwa panga.

Mganga wa zamu wa Kituo cha Afya cha Katoro, Dk. Daneil Izengo, alithibitisha kuwapokea mama na watoto wake hao kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi na wa kiume kwa matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, hakupatikana   kuzungumzia tukio hilo.

Naye  Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Omary Mangochie, alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema polisi walikuwa hawajamfahamisha rasmi.

Hata hivyo, Mangochie aliahidi kufuatilia ili waliohusika wasakwe na kukamatwa kisha kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.
kwa hisani ya  NIPASHE

Related Posts:

  • Rape victim shot dead in court as she was due to give evidence against local 'godman' in India Victim, 25, fighting rape case against Govindanand Teerath for two years Shot as she arrived at court in India to give statement against 'godman' Her mother was injured in the shooting and is now recovering in hospital … Read More
  • KATIKA hali ya kushangaza, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Dorah Joseph (34) anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kutuhumiwa kumfunga mnyororo mtoto wa kaka yake aitwaye Happy Joseph (13) na kumtelekeza bila … Read More
  • Abakwa kwa amri ya wazee wa kijiji India Mshukiwa wa kitendo cha ubakaji Polisi nchini India wamewakamata wanaume 13 waliohusishwa na genge la wanaume waliombaka msichana mwenye umri wa miaka 20 katika jimbo la Benghal Magharibi. Inadaiwa wanaume, hao walim… Read More
  • Athari za dawa ya Saratani zamtuma kuua Jean na Sarah walipatikana wakiwa wameuawa nyumbani kwao Mwanamume mmoja anayeugua Saratani nchiini Uingereza, amefungwa jela maisha baada ya kumuua mkewe na mtoto wake msichana kutokana na athari za madawa anayotumia kwa… Read More
  • Mtanzania abakwa, afa China CHINA AMA kweli dunia hadaa, ulimwengu shujaa! Kumeibuka mchezo mchafu, kuna Watanzania wanawachukua warembo nchini na kuwapeleka China kwa ahadi kwamba wanakwenda kufanya kazi saluni, wakifika kule wanawanyang’anya pa… Read More

0 maoni: