Tuesday, 12 November 2013

Wanalipwa kwa kunyonyesha watoto Uingereza

Akina mama waliojifungua watoto nchini Uingereza wanalipwa hadi pauni miambili kuwanyonyesha watoto wao. Huu ni mradi mpya ulioanzishwa nchini Uingereza kwa usihirkiano kati ya serikali na watafiti wa utabibu, katika mitaa ya Yorkshire Kusini na Derbyshire, ili kuwahamaisha akina mama umuhimu wa kuwanyonyesha wanao wachanga.

Mradi huo pia unatarajiwa kufanywa katika eneo lengine la tatu katika mradi ambao utawalenga akina mama 130 watakaojifungua watoto kuanzia sasa hadi mwezi Machi mwaka ujao.
Ikiwa mradi huu utafanikiwa basi huenda ukafanyika kote nchini Uingerezea, mwaka ujao.
Mradi huu wa kutumia pesa kuwahamisha akina mama kunyonyesha watoto wao, sio mpya nchini Uingereza.
Umewahi kujaribiwa katika kuwahamisha wavutaji sigara kuacha tabia hiyo na watu wanene kupata lishe bora.
Lakini hii bila shaka ni mara ya kwanza kuwalipa akina mama kuweza kuwanyonyesha watoto wao.
Katika mradi huo, akina mama kutoka katika maeneo fulani ya Sheffield na Chesterfield watepewa vocha zenye thamani ya pauni miambili, ambazo wanaweza kutumia katika maduka makubwa na ya kifahari kununua bidhaa.
Maeneo hayo, yameteuliwa kwa utafiti huu kwa sababu akina mama hawawanyonyeshi kabisa watoto wao.
Imegunduliwa kuwa ni mama mmoja tu kati ya wanne anayenyonyesha hadi wiki ya sita ikilinganishwa na sehemu zengine nchini humo.
Ili kupata vocha hiyo, mama atalazimika kumnyonyesha mwanawe hadi miezi sita
Wakunga na maafisa wa afya watahitajika kuhakikisha kuwa wale wanaoshiriki kwenye mradi huo wanapata pauni miamoja na ishirini ikiwa watanyonyesha kwa wiki za kwanza sita.
Mradi huu umetokana na tofauti zilizopo za kiafya , utafiti ukionyesha kuwa kuwanyonyesha watoto kunasaidia kuzuia matatizo ya kiafya kwa watoto kama kuumwa na tumbo, maradhi ya kifua pamoja na kuwasaidia watoto kiakili.
Daktari Clare Relton, mmoja wa wataalamu wanaohusika na mradi huo amesema kuwa anatuami mradi huo utawasaidia wanawake kuona umuhimu wa kunyonyesha watoto wao.
Chanzo - BBC Swahili

0 maoni: