Wednesday 18 September 2013

CHADEMA wameliona la Balozi wa CHINA tu? vipi kuhusu SHIBUDA?


Ni kiwewe lakini ni pia ni woga mkubwa na kutokujiamini kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa hatua yake iliyochukua ya kuandika barua serikalini, ubalozi wa china na kisha Umoja wa Mataifa baada ya kuchukizwa na kitendo cha balozi wa china nchini kuhudhuria katika mkutano wa hadhara wa Chama Cha Mapinduzi.

Kwa kitendo hicho chadema wameonyesha udhaifu mkubwa katika kujisimamia kama chama lakini pia katika kuzisimamia sheria za nchi na kuzifuata, ni udhaifu kwa maana kosa kama hilo ambalo wametaka balozi aadhibiwe, amelifanya pia mwanachama wao, Mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi, John Magale Shibuda Mheshimiwa. Ambapo katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi wa tarehe 15 sept, 2013 katika uwanja wa stendi kuu ya Mwanhuzi, wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu shibuda alisimama pamoja na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhutubia umma wa wasikilizaji.

Tena Shibuda alienda mbali zaidi na kuifanyia kampeni ya wazi CCM kwa kusema kuwa "Chama cha mapinduzi ndicho chenye uwezo wa kuleta Maendeleo kupitia utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi" kauli ambayo tafsiri yake ni kuwa anakubaliana na Ilani ya CCM na anaifurahia na kuishabikia kasi ya utekelezaji wa Ilani hiyo.

Nasema ni Double standard at its maximum kwa viongozi wa CHADEMA kujifanya hawajamuona wala kumsikia SHIBUDA na kuibukia kwenye media wakilaumu hatua za Balozi ambaye kimsingi hawana mamlaka ya kumchukulia hatua bali wataishia kulalamika na kuviomba vyombo vingine vya nchi na kimataifa kumchukulia hatua, lakini wanamuacha mtu amabe wanaweza kumjadili na kumchukulia hatua WHAT A DOUBLE STANDARD..? Tena kwa kosa hilo hilo tena sio mara yake ya kwanza kufanya hivyo. 

Hapo ndipo wenye akili sawasawa wanajiuliza juu ya msukumo walioupata CHADEMA mpaka kufanya maamuzi hayo, ni kweli kuwa yanatokana na fikra zao na mitazamo yao au ni kutoka kwa akili na amri za wafadhili wao ambao wanaona CHINA kuwa ni Adui yao hivyo wanataka kutumia kila njia kuona adui huyo anabanwa ipasavyo..?? na wakaona kuwa chadema wanafaa kutumika katika hilo.

Mimi nasema sio CHADEMA, wala sio Mawazo na Fikra zao bali ni Amri na Msukumo kutoka katika mataifa yaleyale tunayoyazungumza siku zote na kuwa Chadema inaendeshwa kwa remote control kutoka kwa mataifa hayo. Ikiwa Chama kinafikia hatua hii kuwa hakiwezi kufanya maamuzi wala movement yeyote isipokuwa ile ambayo wameagizwa na mataifa hayo ya nje ni Hatari kubwa kwa Chama na wanachama wake lakini hatari hiyo ni kubwa zaidi kwa wananchi.

CHADEMA shame on you..,viongozi wa Chadema acheni kutumika ni aibu na dharau kubwa...!


Kwa hisani ya - "TandaleOne"

0 maoni: