Sasa naamini kuwa kuna mkakati wa serikali ya JK kuislamisha nchi hii. Nimeingia na kiberenge changu asubuhi ya leo kumwona mgonjwa aliyelazwa pale. Nikakuta askari wa pale wameziba sehemu ya kuingilia magari kwenda kupark...nikazungusha kwenye mduara kisha nikaamua kumfuata yule aliyeziba ambaye alikuwa pale wakati napita mara ya kwanza akanitazama kama nyanya mbovu. Baada ya kumwangalia kwa jicho kali akanifungulia...hamadi mbele yangu nikakuta jopo kubwa la watu wanaovaa suruali fupi na vikofia wako kwenye mduara mkubwa huku mmojawapo akitoa maelekezo.
Kuna baadhi yao walikuwa kama hawajiamini...kila mtu anayepita jirani walimuangalia kana kwamba wanataka kumtoa roho. Nikapaki gari na kuelekea wodini...nilichokikuta huko nako ni haohao jamaa wa kike na wakiume wamevalia mavazi maalum. Nikauliza kulikoni jamani maana mimi sijaja hospitali siku nyingi! Imekuwa hospitali ya kiislamu au umekuwa ni msikiti? Aliyenijibu akaniambia hawa jamaa hata Muhimbili wako kule siku hizi, humpa kila mgonjwa andazi moja na kikombe cha uji asubuhi. Nikasema hiyo ni huduma nzuri...lakini cha kushangaza mbona wako wengi sana na wanaonyesha kuwa na sura za wasiwasi na kutojiamini hasa wale waliokaa mduara? Nikauliza na wakristo wakitaka kufanya hilohilo wataruhusiwa na kupewa ulinzi na hospitali kama hawa? wapagani je? waganga wa kienyeji? Nikagundua ni kweli serikali yetu inaweza kuwa na upendeleo kwenye maeneo fulani au inaweza ikawa inawaogopa hawa jamaa. Ukweli ni kuwa hawa jamaa wanaonyesha wako kimkakati na kama wanapanga mambo yao kwa nini wasipanhie mambo yao msikitini na kuja kutoa tu huduma? nna wasiwasi iwapo vyombo vya dola vitaachia mambo haya yaendelee...sijui! yangu macho.
Mdau - Mkulima wa Kuku
0 maoni:
Post a Comment