Friday 8 February 2013

Bob Junior afunguka kuhusu kuoa mapema


Msanii maarufu wa muziki wa  kizazi kipya almaarufu kama Bob Junior ambae pia ni mtayarishaji wa muziki amefunguka kuhusiana na sababu ya yeye kuweza kuchukua uamuzi wa kuoa mapema. Mr. Chocolate Flavour alifunguka na kusema kuwa sababu iliyomfanya kuchukua uamuzi huo wa kuoa ili aweze kujenga maisha yake na pia kupunguza idadi ya marafiki wasio na umuhimu katika maisha  yake na kusema kuwa rafiki yake wa ukweli kwa sasa ni mke wake tu kwani ndiye anayeweza kumshauri vitu vizuri.
Bob alisema kabla hajaoa alikuwa anaishi maisha ambayo ni hatarishi, kushinda vijiweni na kuwa na marafiki wengi ambao walikuwa ni hatarishi katika maisha yake. Mbali na hayo mwanamuziki huyo aliongeza kwa kusema kuwa ameoa mapema kwasababu yeye ni mtoto wa kiislamu na amelelewa katika maadili ya dini hivyo sheria ya dini inamruhusu mtoto wa kiume kuoa pindi anapobalehe.


0 maoni: