“Wataalamu wetu wamejitahidi kutoa huduma kwa mgonjwa huyu kufikia kiwango cha kuweza kuongea mwenyewe na kujitambua vizuri.
“ Changamoto tuliyonayo ni kuwa mgonjwa huyu tangu alazwe hakuna ndugu wala jamaa yake yeyote aliyejitokeza. Hivyo kwa sasa tunatafuta ndugu wa mgonjwa huyu ambaye amepata nafuu ili aweze kujiunga na familia yake,” alisema Aligaesha.
Alifafanua kuwa katika kufanya udadisi imegundulika kuwa Esther alizaliwa Kigoma vijijini katika Kijiji cha Kigogwe mwaka 1985. Kabila lake ni Muha na anasema mama yake anaitwa Dotto Alfred na baba yake anaitwa Meshaki Alfred ambao hata hivyo, walitengana.
“Ndugu, jamaa au yeyote mwenye taarifa za mgonjwa huyu naomba awasiliane na Ofisi ya Uhusiano Hospitali ya Muhimbili kupitia namba 0755 648 636,” alisema afisa habari huyo.
No comments:
Post a Comment
Toa ushauri wako au andika chochote hapa ... Leave your comment here