Thursday 31 January 2013

Habari zenu Wadau 
Leo nimeona nijiingize tena humu room kwa style ya kutambaa kwa kunyata nyata. Nimekuwa nikijiuliza sana swali hili wala sipati jibu ila nina mtazamo kidogo ninaoufahamu kiasi, Nimeona leo nililete kwenu nanyi mniambie hiyo mada hapo juu inayosema: KATI YA KUPENDA AU KUPENDWA KIPI kinatangulia jamani waungwana. 
Lakini katika mtazamo wangu finyu kidogo nimeona KUPENDA ndiko kunatangulia ndipo linakuja suala zima la kupendwa, ingawaje siku hizi vijana wengi wanachukulia jambo hili simpo kwao na wanaona kitu chepesi sana kwao, La hasha si jepesi kama mnavyofikiri ukiingia ndani zaidi suala hili ni pana na halina mlango wa kutokea. Na ni zaidi ya upana kwani linapelekea kuletea uzao mwingi duniani. na vilevile huleta faida na hasara pia japokuwa sijapata takwimu asilia.


Neno Upendo limegawanyika katika mafungu makuu 3 ambayo ni:
a) Ule upendo wa kimazoea yaani kindugu, kirafiki, kijirani n.k
b) Ule upendo wa nafsi / yaani kujipenda wewe mwenyewe
c) Ule upendo wa Agape yaani kupenda zaidi ya kupenda kama Mungu alivyotupenda na kumleta mwanawe (huu niupendo usio na unafiki wowote ni upendo wa kweli kabisa)

Nimechambua kiasi kidogo lakini kama yuko ambaye anayeweza kuchambua ataongezea hapo. Kwanini leo nimeona nilete mada hii marafiki zangu, kitu kilichonisababisha mpaka kuleta jambo hili kwenu ninataka kuwatia moyo wale ambao wamekatishwa tamaa na wenzao ama ndugu, rafiki, jirani amekuona hufai kabisa na vilevile nimetaka kuwashauri wale ambao wanawapenda wenzao kwa kuwa na vitu.

Siku hizi kumekuwa na wimbi izito la watu kuwa na mazoea mabaya kwa wanadamu kwani wengi wao wanampenda mtu akiwa flesh, au akiwa na kitu, fedha, mali, afya njema n.k. lakini kama huna kitu au u-mgonjwa, hata hao waliokupenda awali wakati ukiwa navyo wanakukimbia na kukuacha na kukuona hufai kitu kabisa, wengine walikuita majina mazito mengi tu kipindi kile ulivyokuwa unavyo uliitwa pedeshee, mama mkubwa, kizito, n.k lakini zilivyopukutika nao wakapukutika kabisa na kukuona kuwa huwezi kitu.

 Kuna kisa kimoja ni cha kweli kimetokea kabisa amekiimba mwimbaji wa nyimbo za Injili Ambwene Mwasongwe ambacho kinaelezea kaka mmoja alivyompenda dada mmoja wakati wa mahusiano yao kuwa vizuri kwa muda mrefu, ghafla yule binti alipata na ukichaa wazazi wake walimpeleka Hospitali lakini hakupona siku moja walimpeleka kanisani kuombewa aliombewa akapona, wakiwa mbele ya madhabahu wazazi wa yule binti wakatoa ushuhuda jinsi binti jinsi binti yao alivyopona waaumini walifurahi ndipo walipomgeukia yule kijana na kuumuliza je utaendelea kuwa na binti yetu? naye bila ajizi alisema nitakuwa naye na ninampenda kweli watu walishikwa na butwaa la mshangao kwa yule kijana kuwa na msimamo wake kumpenda mtu hata kama yuko katika hali ile aliyonayo. Sasa hapo ndipo nasema ndio upendo wa kweli unaopoonekana, Unapenda mtu akiwa katika shida, majaribu na matatizo ndipo upendo wa kweli unathibitika na kuonekana.



Mdau - LadyFurahia

0 maoni: